Monday, 25 July 2016
SURA YA KWANZA (1) AMINI KATIKA IMANI YA KILE UNACHO KIAMINI
Habari za wakati huu vijana na viongozi wenzangu, Napenda kuchukua Fursa hii kabisa kwa moyo mkunjufu kukukaribisha katika mfululizo wa makala mbalimbali katika ukurasa huu. Nipende kuchukua fursa hii kukushukuru wewe unayesoma makala hii. Umefanya uamuzi sahihi sana.
Leo hii naanza na mfano huu, Baba mmoja alikua na watoto wawili, ila mtoto mmoja alikua anahisi kua baba yake ana dhahabu kubwa na ameificha katika sehemu moja wapo ya nyumba yao. Mbele ya nyumba yao kulikua na hekari kumi za shamba. Ilifika wakati baba yao akaugua sana na Kabla ya kufa, baba alisikika akisema, "Hekari kumi!" Hekari kumi!" Hekari Kumi" Moja kwa moja Yule kijana wa kiume alivyosikia maneno hayo akajua fika dhahabu iko kwenye shamba lao. Baada ya kumalizisha mazishi, wakaanza kutafuta dhahabu shambani, wakifyeka na kusafisha shamba, hata baada ya kumaliza hekari kumi hawakupata chochote, Kaka yao mkubwa alipofika akasema, "mmefanya vyema sana, haya na tuoteshe mahindi! Haikua rahisi kumuelewa, kwa sababu walikua wanataka dhahabu na sio mahindi. Ila Baada ya msimu mmoja wale vijana walivuna mazao mengi ambayo kwa baba yao ndo ilikua dhabu yake! (moral of the story, it is the combination of mindset and the process that will lead to good outcome)
Kuna nguvu katika imani ya kile unacho kiamini. Chochote tunacho kifanya lazima uwe na imani nacho, Kubali ukweli kwamba itachukua muda lakini amini kua lazima kitokee unacho kiamini. Watu wengi wamekua na mitazamo mizuri lakini hukatizwa na fikra zilizojaa uoga (fear) hivyo kutofikia yale ambayo wanayaamini. Kila kitu huchukua muda na amini katika muda. Usikatishwe tamaa na mazingira, marafiki, ndugu kwamba huezi fikia jambo ambalo unaliamini.
Jack Ma founder wa Alibaba.com katika ten Principles of SUCCESS aliwahi kusema kua, get used to rejections, kubali kukataliwa, sio kila mtu ataamini kile unacho kifikiri wala unachosema na usitake waamini kwa sababu ipo siku wataamini bila hata kuwaambia.
Hivyo napenda kukutia moyo, kua na imani ya kile unacho kiamini, Kama ni Mahusiano, Just amini tu kwamba kuna wanaume wazuri wengi wapo na wanawake wazuri wapo, Kama ni kazi fanya kazi tu ana amini katika kufanikiwa, Kama ni kupata kazi amini tu kwamba utapata na utafanikiwa, Kama ni mke mwema amini tu kua utapata hata kama itachukua mda. Kinachowatokea wengi ni kua Huamini katika kushindwa na uoga, Uoga unapotawala mawazo yako unakuletea mitazamo hasi (negative emotions) ambazo zikizdi basi hutawala mitazamo chanya uliyo nayo (positive emotions). Hi husababisha kupoteza mwelekeo wa kile unacho kiamini na uoga unakua ugonjwa wako wa akili (mental disease) kutokana na namna uoga ulivyokuzoea.
Hivyo napenda kumalizia kua kuna nguvu na siri kubwa katika kuamini, Mafanikio yako yanatokana na namna unavyofikiri. Kila siku kua na mitazamo ya ushindi na hilo ndo litakua nguvu yako. Kumbuka kila mtu ni kama mgodi wa madini, Kila mtu ana madini ghali hivyo ni nmna gani ya kuyatumia madini uliyo nayo. Hakuna madini yanayopatikana kirahisi, inahitaji mbinu, na kuamini kua kuna madini ndani yako tena madini ghali kabisa. Hivyo usikatishwe na Umbali wa kupata hayo madini ila jua yako ndani yako na lazima uyapate!!
Uwe na wakati mzuri katika kulijenga Taifa! unaweza kuacha maoni yako au kufollow hii page kwa njia email!
Ni mimi kijana mwenzio na Mwalimu wako Erick Mramira!
AMINI KATIKA IMANI YA KILE UNACHO KIAMINI!!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)

