Thursday, 29 September 2016

UCHAMBUZI WA KITAB: STUNNING ON SUCCESS BY SHARMAS. SEHEMU YA PILI

Ni matumaini yangu kuwa u zima wa afya tele, na unaendelea vyema na majukuamu yako ya kila siku katika ujenzi wa taifa na ujenzi wa maisha yako ya kila siku.
 Siku zote hakuna furaha zaidi ya ile ambayo uko nayo, furaha huja kwa kupenda kile unachofanya, kupenda nafasi uliyo nayo, kupenda kazi uliyo nayo. 
Uamuzi ni wako wa kua na furaha au kutokua na furaha, wengi husema nitakapokua na mali nying nitakua na furaha au nitafanya kila kitu au nikiwa na familia kubwa nitakua na furaha, au nikipata kazi nitakua na furaha. Ila nipende kukutia moyo kua we ndiye the C.E.O of your own happiness. Wanazuoni wanasema 
  "Own your happiness" 
Hivyo furahia kila wakati ulio nao kwani huo wakati ndio furaha yako.
  Nipende kukukaribisha katika sehemu ya pili ya makala ya uchambuzi wa kitabu kutoka kwa mwandishi nguli Robin Sharma's. Kabla ya Kuendelea na uchambuzi wa kitabu chake, tuangazie baadhi ya nukuu (quotes) zake zilizowahi kujizolea umaarufu katika tasnia ya uongozi.(leadership & management).
                    Meaning of stunning for success; Creating an impressive success
            
                                  QUOTE FROM ROBIN SHARMA'S
Public speaking, Robin Sharma's



  1. The secret to genius is not genetics but daily practice married with relentless perseverance.
  1. The best leaders lift people up versus tear people down.
  1. The most precious resource for business-people is not their time. It’s their energy. Manage it well.
  1. The fears you run from run to you.
  1. The most dangerous place is in your safety zone.
  1. The more you go to your limits, the more your limits will expand.
  1. Every moment in front of a customer is a gorgeous opportunity to live your values.
  1. Be so good at what you do that no one else in the world can do what you do.
  1. You’ll never go wrong in doing what is right.
  1. It generally takes about 10 years to become an overnight sensation.
  1. Never leave the site of a strong idea without doing something to execute around it.
  1. A strong foundation at home sets you up for a strong foundation at work.
  1. Never miss a moment to encourage someone you work with.
  1. Saying “I’ll try” really means “I’m not really committed.”
  1. The secret of passion is purpose.


SEHEMU YA KWANZA (I)WHAT IS LEADERSHIP.Katika makala hii anaanza kwa kuzungumzia "nini maana ya Uongozi" "Kiongozi ni nani" anaanza kwa kusema kuwa. kuwa kiongozi haina mfungamano kabisa na cheo, nafasi, sifa au ukuu flani, au sio ukubwa na size ya offisi. Uongozi si kuwa na hela nyingi au uthamani wa nguo unazo vaa. Anakazia kwa kusema na nukuu" leadership is philosophy,its an attitude, its state of mind, and its available to each one of us." Kiongozi ni tabia, uongozi ni namna unavyofikiri, uongozi ni kitu ambacho kila mtu alibarikiwa kuwa nacho. 

Uongozi is ni kuwa responsible, be accountable, bila kujali nafasi, cheo au u boss wa mtu, Kila mtu alizaliwa kiongozi. Katika ofisi yeyote, kila mtu ni kiongozi, uongozi hujionyesha pale mtu anapokua responsible na nafasi aliyopewa, kufanya kazi yako kwa umakini kunaonyesha nafasi ya uongozi katika nafasi unayo fanya. 


Matokeo yeyote katika taasisi yeyote ni matokeo ya uongozi uliofanywa na kila mtu katika taasisi. Bila kujali cheo, au uboss wa mtu yeyote.Hivyo napenda kuhitimisha katika eneo hili kuwa kila mtu ni kiongozi, kila mtu ana namna ya kudhihirisha uongozi wake bila kujali nafasi, cheo au utajiri wa mtu. Niseme tu, leadership is about responsibility, its an attitude, and each one of us was blessed with.                            

 What will you do to be the leader that you are destined to  be, today?                     
(II)WORLD CLASS LANGUAGE.

Kitabu hiki "little black book on stunning for success" ni mtiriko wa vichwa mbalimbali ambavyo vimezungumziwa katika kitabu hiki. Hivyo tutachambua angalau vichwa(titles) mbili kila siku. Mwandishi katika word class language anajaribu kuzungumzia lugha na mtazamo ambao mtu anakua nao. 
Siku zote maneno yana nguvu sana, ukiamini katika maneno ya kushindwa basi hakika utashindwa ila ukiamini katika lugha ya fursa , nafasi, ushindi basi utafanikiwa sana. mwandishi anasema, tuna uamini na kuulewa ulimwengu kupitia maneno,maneno unayoyatumia yanaelezea namna unavyo iona hali halisi.

Nukuu  (quotes)     

   If you call a stumbling block a “problem” or “a big mess” you will create a different emotional state within you than if you call the issue “an opportunity” or “a challenge that will only make me better. 

        kama ni fursa au changamoto, ni vile ambavyo unavyoielezea, kama ukiamini kila kitu ni tataizo basi akili hujenga mtazamo tofauti ila ukiamini katika fursa basi kuna nguvu ndani yake. ("Uwezo wa kutatua tatizo si ukubwa wa tatizo bali ni namna unvyolielewa tatizo Erick 2016")kinachowatofautisha watu ni namna wanavyoongea na kuzungumza, watu waliofanikiwa huzungumza lugha za uvumilivu, lugha za fursa, lugha za ushindi lugha za uongozi, lugha za upendo. hivyo ni kweli kabisa tunapitia katika changamoto nyingi, wakati mwingine unakosa ufumbuzi, wakati mwingine unaona tatizo ni kama jabali kubwa ambalo huezi kulisogeza. Nipende kukuambia kua haijalishi ukubwa wa tatizo, jijengee uwezo wa kuamini katika lugha za mafanikio, fursa, hii ndo njia ya kusogeza jabali kubwa ulilo nalo......


Nipende kukushukuru sana wewe uliyechukua nafasi kupitia makala hii, utabarikiwa sana. Naamini hadi mwisho wa kitabu utakua umejifunza mengi. Endelea kutembelea makala hii kila siku. Kwa kusoma makala hii wewe ni wa pekee sana...
     

Imedhaminiwa na  
Youth developmnet and empowernment & kijana kwanza Iniatives.                      Kmeandaliwa na Mwandishi Erick mramira            (Mwanzilishi wa YEDO na Kijana kwanza Initiatives)                               ....................itaendelea...........................................