SEHEMU YA PILI (2) UTOFAUTI WAKO UNAKUTOFAUTISHAJE?
Habari za wakati huu kijana na msomaji wa makala hii kutoka katika tovuti ya mendeleo kwa vijana. Ni matumaini yangu kua ni mzima wa afya na unaendelea kutekeleza majukumu yako ya kila siku. Nipende kukutia moyo tu amini katika kile unacho kifanya, Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema hatuwezi kubadilisha hali ilivyo ila tunaweza kubadilisha mcho yanayo ona hali halisi ( we can not change the reality but we can change the eyes that see reality)
Katika makala ya leo tutaangalia umuhimu wa kua tofauti, nnaposema tofauti namaanisha namna ambavyo watu wengine wanakuona. Ili uweze kuonekana tofauti lazima wewe mwenyewe utengeneze utofauti ndani yako. Kila mtu yuko vile alivyo na hakuna hata mmoja anafanana na mwingine.Ukiona tabia zako zainafanana na mwingine basi jua bado hujatambua utofauti wako.
Nataka nikuambie kuna nguvu katika kua tofauti, Mtu mwenye tabia flani, huhitaji nguvu sana kumtambua. Utofauti wako ndio unakufanya uishi au ukae na jamii flani, hivyo kua tofauti kuna fanya uambatane na makundi flani. Hivyo basi utofauti wako huambatana kwa kiasi kikubwa na tabia yako, Maisha yako ya kila siku yanatengeneza utofauti wako. Wakti mwingine unajikuta un associate na watu wengi pasipokukujua nini kinafanya wawe karibu na wewe. Kua karibu na watu hauhitaji pesa au cheo ili ufahamike, hata kama huna pesa au mali kunaweza kusababisha wewe kukutana na watu wa tofauti kulingana na utofauti wako. Tunapaswa kua na utofauti ambao unaweza kukutambulisha kwa watu bila wewe kujitambulisha. Utofauti wako unaweza kukutanisha na fursa ambazo ulikua hutarajii kukutana nazo. Utofauti huo ndio unasababisha promotion(kupandishwa cheo) au kutunukiwa heshima mbalimbali. Utofauti wako ndio utakukutanisha na viongozi mbalimbali na watu wengine wenye hadhi tofauti. Naamini kila mtu ana kitu cha tofauti ambacho kwa hakika kinaweza kukutofautisha na mwingine. Tunapaswa kutambua utofauti huo na kuanza kuufanyia kazi.
SOMO KATIKA TOVUTI: FANYA MAAMUZI SAHIHI
Nipende kukutia moyo rafiki na msomaji wa makala hii kua, popote pale unapaswa kuonyesha utofauti wako ambao utakutambulisha kwa watu wengine. Inategemea ni utofauti wa namna gani ambao unataka kua nao. Kama ni utofauti wa mindset au fikra basi watu wakutambue kwa utofauti huo na namna ya kufikiri kwako kuwe tofauti kabisa na wengine. Kama ni tabia basi watu wakutambue kwa tabia yako. Kama ni proffessionals au career yako basi jenga utofauti katika hilo ili uweze kua tofauti na wengine na wao waeze kutambua utofauti wako. Nikukumbushe tu kua utofauti wako unaeza jenga na kutengeneza kitu kikubwa sana. Napenda kumtumia Jack ma ambaye ni Founder wa Alibaba.com. Kilichomsfikisha hapo alipo ni namna alivyoweza kufikiri kwa tofauti na katika utofauti wa fikra zake ameweza kutofautishwa na makumpuni mengine ambayo yanafanya kazi sawa na yake. Hiyo ni nguvu ya kua na fikra tofauti ambazo zimeleta mabadiliko na tofauti kubwa katika ulimwengu wa online business au biashara kwa njia ya mtandao.
Tatizo lilopo kwa sasa, kulingana na utandawazi na mbadilko katika ulimwengu wa sasa, tunajikuta wote tunataka kufanana na ulimwengu huo, ila kama tuko tayari kutumia mabadiliko hayo basi tutakua tofauti sana katika ulimwengu huu wa mabadiliko. Kila kitu kina badilika, mtoto anayezaliwa sasa hivi haezi jua kama kulikua na tape au kanda kwa sababu amezaliwa zama za CD na DVD, haezi jua kama watu walikua wakitumia tv za chogo kwa sababu amezaliwa zama za flat Screen. Nini kinafnya haya yote, Ni utayari wa watu wachache walioamua kua na utofauti wa kifikra na wakafikiri kwa namna ya utofuti na ndo maana leo hii tunaona utofauti wao.
Katika kila jambo unalolifanya jaribu kua tofauti, wote tunaeza kua na jibu sawa lakini njia za ukokotoji zikatofautiana. Tusitamani wote kua na njia moja bali njia zetu zitofautiane ili tuonyeshe utofauti. Nipende kusema tuu, Utofauti wako ni wa muhimu sana cha kufanya ni kujaribu tu kuufanyia kazi ili uwe wa kitofauti.
Kuchukua muda wako na kusoma makala hii, WEWE NI WA TOFAUTI SANA, Utayari wa kusoma hii blog ina maanisha mawazo yako yana utofauti na unataka kua tofauti kwa kuongeza maarifa tofauti, YOUR the Best!
Nipende kukushukuru kwa kuchukua muda wako na kusoma makala hii!
Unaweza kuacha maoni yako au kuendelea kusoma makala mbalimbali katika tovuti hii! Makala hii imeandaliwa na
Erick MramiraMwezeshaji na mpenda maendeleo kwa vijana
www.youthdevelopment22.blog spot.com
Kijana kwanza!

No comments:
Post a Comment